Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa Mpango kabambe wa Sekta ya Uvuvi utasaidia kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka kutoka asilimia 1.8 ya sasa. Pia amesema kuwa mpango huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia 2021/2022 hadi 2023/2037 una umuhimu mkubwa katika ukuaji wa sekta ya uvuvi pamoja na uchumi wa bluu.