MAKALA

MRADI WA KUZALISHA SAMAKI AINA YA KAMBALE MUMI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KATIKA BONDE LA ZIWA VICTORIA

20/10/2017

UTANGULIZI

Awali ya yote tunapenda kuchukua nafasi hii kukumbusha kuwa Mradi huu ni matokeo, baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua Mpango wa KILIMO KWANZA mnamo Tarehe 3 Agosti 2009, ukiwa na lengo la kukuza Sekta ya Kilimo ili iweze kupata msukomo zaidi katika kupunguza umasikini na kuleta maendeleo ya haraka. Katika kuitikia azma hii, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) ilibuni Mradi wa kuzalisha vifaranga vya samaki aina ya Kambale Mumi (kwa kitaalam Clarias gariepinus) kwa wafugaji wa Samaki ili wananchi waweze kushiriki katika kujipatia maendeleo yao na hivyo kuondokana na umaskini.

Historia Fupi ya Uanzishwaji wa Mradi wa Kuzalisha Kambale Mumi (Clarias) Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko la soko la samaki aina ya Sangara (Nile perch) kwenye soko la Kimataifa na hapa nchini. Hii ilileteleza ongezeko la uvuvi wa migonzo/ndoano kwa wavuvi wadogo wadogo (ambao ndio wengi) ambao hutumia Furu au Kambale Mumi wadogo("Neke") kama chambo cha kuvulia Sangara.

Uvuvi wa Sangara kwa kutumia Mumi wadogo kama chambo kuchagiza kuvuliwa kwa samaki wenye uzito mkubwa. Hivyo wavuvi walihamasika kuongeza pato lao kiuchumi kupitia uvuvi huu. Kwa sababu hizo za kiuchumi, chambo aina ya Mumi wachanga walitafutwa maeneo mbalimbali kama vile kwenye mito na vijito, kwenye mazalia, au hata kwenye madimbwi. Hali hii imesababisha uharibifu mkubwa hasa katika Maeneo oevu (Wetlands) na Maeneo chepechepe (Marshlands) kwa uchimbaji holela. Hivyo basi, Mumi waliopo kwenye maeneo haya walitishiwa kutoweka kutokana na mahitaji kuwa makubwa. Kwa sababu hizi kulikuwa na haja ya kutafuta njia mbadala ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira, na hapo hapo kupata njia mbadala ya kupata chambo ili kuwa na uvuvi endelevu wenye tija na kuongeza kipato kwa Wananchi kupitia Mpango wa maelekezo yaliyoainishwa kwenye misingi ya Kilimo Kwanza. Kwa hivyo basi, lengo kuu la Mradi huu ni kuwapatia wanavikundi teknolojia rahisi watakayoweza kuimudu katika kuzalisha kwa wingi vifaranga vya Mumi ili kukidhi mahitaji.

Sifa zinazomfanya Kambale Mumi kuwa chaguo sahihi kwa Mradi wa kuwazalisha Kambale Mumi ambao hujulikana kwa jina la kitaalam kama Clarias gariepinus ni aina mojawapo kati ya aina nne za jamii ya Kambale zinazopatikana katika bonde la Ziwa Victoria. Wenyeji humwita "Kombati" kutokana na mwonekano wa ngozi yake. Aina hii ya Kambale hupevuka anapokuwa na urefu kuanzia sm 30 na huweza kukua hadi kufikia urefu wa sm 170. Aina nyingine za Kambale Mumi wanaopatikana katika bonde la Ziwa Victoria hawakui kwa kiasi kikubwa namna hii. Hawa ni wale wanaojulikana kitaalamu (na urefu wao wa ukomo kwenye mabano) kama Clarias liocephalus (sm32); Clarias alluaudi (sm35), na Clarias werneri (sm 23).

Hivyo Kambale Mumi (Clarias gariepinus) ana sifa za ziada kwenye ufugaji wa samaki. Isitoshe, sifa za ziada kimaumbile humwezesha kuvuta hewa kavu na wakati mwingine kuishi kwenye tope nzito, au kuvuta hewa kwa kutumia mdomo. Samaki huyu anapotumika kama chambo hukaa kwenye ndoano kwa muda mrefu bila kufa. Na kwa vile samaki aina ya Sangara huwa hali samaki mfu (mzoga), nafasi inakuwa kubwa ya kukamatwa Sangara anayelengwa. Kambale jike hutoa mayai yaliyokomaa tayari kwa kurutubishwa kuanzia 36,000 hadi 650,000 (kutegemeana na ukubwa wa samaki) na dume hutoa mbegu nyingi zaidi ya idadi hiyo ili kuwezesha mayai kurutubishwa. Homoni sanisi (synthetic hormone) au tezi ubongo au 'pituitari' (pituitary gland) hutumika kumdunga samaki jike kwa ajili ya kupevusha mayai ambayo hutolewa kwa kukamuliwa na kuchanganywa na mbegu ili kurutubishwa na kisha hutotoleshwa.

Andiko la Mradi Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) ilibuni Mradi huu wa kuzalisha vifaranga vya Kambale Mumi kupitia Kamisheni Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Mradi huu ulipata takriban Shilingi milioni 150 kutoka serikalini kwa kazi ya kipindi cha miaka mitatu (katika utekelezaji wa Nguzo na. 2 ya Kilimo Kwanza - kutenga mafungu ya bajeti kwa vikundi vya uzalishaji). Hivyo basi Lengo kuu la Mradi huu ni kutotolesha vifaranga vya Mumi kupitia teknolojia ya ufugaji wa samaki ili kutekeleza sera ya Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) na hapo hapo kuhifadhi mazingira katika bonde la Ziwa Victoria.

Aidha, Mradi unalenga katika kuzalisha Mumi wengi zaidi ili kupata mbegu bora kwa ajili ya kukuzwa kwenye mabwawa ya kufugia samaki. Hivyo wanakikundi wafugaji watakuwa na uwezo wa kipato kutokana na vifaranga walivyozalisha na kuviuza kwa ajili ya matumizi ya chambo kwenye uvuvi wa Sangara, na pia kurahisisha upatikanaji wa mbegu kwa wafugaji wenye mabwawa ya kufugia samaki.

EMIL GEOFREY 20/10/2017 09:38:59 AM
ninaupongeza sana mradi huu wa kuzalisha kambale sababu ktk ufugaji swala la vifaranga hasa vya kambale ni moja ya changamoto kubwa sana,Lakini je sisi kama wadau ktk swala hili tunaruhusiwa kutembelea mradi?Reply
SAILALE 02/09/2017 16:56:47 PM
haswaa unaruhusiwa kutembelea mradi na kujifunza wasilanana na amonshoko@tafiri.go.tz Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:42:36 AM
Karibu sana sana Reply
LESPREMIA 01/04/2019 09:45:15 AM
Viagra On Line Forum Cialis 20mg Lilly Acheter Propecia Scotland acheter priligy au canada Cialis Da 5 Mg Prezzo Reply
AMIN 02/05/2016 09:12:08 AM
Soko la kambale likoje? Hapo ndio penye changamoto Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:38:36 AM
Soko la Kambale sio Gumu, kwani kambale huweza kukaushwa na kusubiri soko Reply
KARIMU NGAJIME 02/09/2017 16:19:30 PM
mimi npo mtwara nawezaje kupata vifaranga wakiwa hai, natamani niingie kwenye huu mradi Reply
STEVEN ERIC 02/09/2017 16:22:31 PM
NzuriReply
COSTANTINE MAUNJO 05/02/2017 09:27:20 AM
Samaki aina ya kambale wa kufugwa ndani ya miezi minane anakuwa na uzani gani? Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:37:47 AM
Inategemeana na Bwawa, Ubora wa Maji, Ubora wa mbegu, Ubora wa Chakula, Uzingaliati wa usafi wa maji na muda wa malisha n.k karibu ofisini kwa maelezo zaidi Reply
PHILBERT MTEY 13/02/2017 12:41:08 PM
Naweza kipata vifaranga wa kambale?na bwawa la sq m10*10 linauwezo wa kuchukua vifaranga wangapi?Reply
PATROBA ERASTO 13/02/2017 10:36:19 AM
mradi mzuri. nitawatafuta ili kujifunza zaidi. Reply
NICKSON MUGASHA 19/02/2017 08:43:52 AM
kwenye bwawa la sq 10x10 wataingia Kambale 1000Reply
FADHILI LUNGOLE 11/05/2017 01:57:18 AM
Mimi napongeza huo mradi wenye kuleta maendeleo katika nchi yetu. Je Ni wapi mlipo kwaajili ya mafunzo kwa sisi tunaotak a kujua jinsi ya kufuga samaki.!? Reply
PATRICK NYEMO 28/07/2017 02:51:53 AM
Naomba namba zenu za simuReply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:39:58 AM
(+255) 22 265 0043 Reply
JAPHET 06/08/2018 11:58:33 AM
hiyo hormoni ya kutotoleshea hao mumi mnanunua au mnatengeneza wenyeweReply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:34:04 AM
Tunatengeneza na nyingine tunanunua ili kufananisha ubora Reply
ASHRAFU HIJA KWANGAYA 19/08/2019 09:11:18 AM
kazi nzuri nipo Dar es salaam nahitaji vifaranga naomba mnisaidie mawasiliano ya mtu wa Dar anaeweza kuniuzia 0746 969393. Shukran.Reply

Leave your comment here

Your comment will be posted after it is approved.
Name(required)* E-mail(optional)
Comments(required)*
Notify me of new comments to this post by email