TAFIRI KUZALISHA PROTINI ZA SAMAKI KWA WAKAZI WA VIJIJINI KUPITIA MRADI WA INNOECOFOOD

Leo tarehe 16 Januari, 2024, Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) yalishuhudia uzinduzi rasmi wa mradi wa INNOCOFOOD, ambao unaleta matumaini mapya kwa maendeleo ya kilimo cha samaki na uzalishaji wa protini vijijini.

Mradi huu wa kipekee unalenga kuboresha uzalishaji wa protini muhimu kama samaki (sato na kambale), mwani (spirulina), na hata wadudu kama vile Black Soldier Fly na cricket, ambazo zina thamani kubwa katika lishe. Lengo kuu ni kuongeza upatikanaji wa protini bora kwa wakazi wa vijijini.

Teknolojia za kisasa za ufugaji samaki kama vile IPRS (Integrated Poly-culture Recirculating System) na RAS (Recirculating Aquaculture System) zitatumika kwa ufanisi mkubwa katika mradi huu. Aidha, mbinu za ufugaji wa wadudu kupitia vizimba pia zitatumika.

Licha ya matumizi ya teknolojia, mradi huu utasaidiwa na akili bandia (AI), ambayo itasaidia kufanya maamuzi ya kiufundi na kuhakikisha kuwa uzalishaji unaendelea kwa ufanisi mkubwa.

Uzinduzi huu unaashiria hatua muhimu katika juhudi za TAFIRI za kuleta mapinduzi katika kilimo cha samaki na uzalishaji wa protini vijijini. Tutegemee mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kijacho!

Post a comment