TAFIRI NA CHINA WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU USHIRIKIANO WA UTAFITI WA BAHARINI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) alipokea wajumbe kutoka Taasisi ya Oshenolojia ya Bahari ya Kusini ya China (South China Sea Institute of Oceanology, Chinese Academy of Sciences, SCSIO-CAS). TAFIRI na SCISIO-CAS walijadili ushirikiano katika maeneo tofauti ya utafiti kwenye Ukanda wa Bahari ya Hindi, pamoja na mafunzo katika sayansi ya bahari, oshenolojia, ikolojia ya bahari, na tathmini ya bioanuwai. Profesa Weiqiang Wang, Mkurugenzi Mkuu wa SCSIO-CAS, aliongozana na watafiti watatu, huku uongozi wa TAFIRI ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Utafiti na Uratibu, na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za makao makuu ya TAFIRI jijini Dar es Salaam, tarehe 11 Aprili 2024.

Post a comment