TAFIRI YASHIRIKI MKUTANO WA KIKUNDI KAZI CHA BIOANUWAI

Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Bw. Hilary Mroso (kwanza kulia) akifuatiwa na Dk. Shechonge (Wa pili kutoka kulia), wakiwa na washiriki wengine wamewakilisha Tanzania katika Mkutano wa Kikundi cha Kazi cha Bioanuwai cha Mamlaka ya Kuhifadhi na Usimamizi wa Ziwa Viktoria (LVFO) kuhusu Uzalishaji wa Samaki, Jenetiki, na Usimamizi wa Bioanuwai uliofanyika huko Mombasa, Kenya, tarehe 15 - 16 Aprili 2024.

Pia Mwenyekiti wa kikundi kazi cha kikanda cha LVFO & TRUEFISH Technical team, Dk. Asilatu Shechonge, alitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa TRUEFISH (utafiti wa uchunguzi wa jenetiki) katika kikao hicho, ambapo walipitia ripoti ya mradi huo na kuandaa mapendekezo ya kisera katika sekta ndogo ya Ukuzaji Viumbe Maji katika Bonde la Ziwa Victoria.

Post a comment