TAFIRI YATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA UMOJA WA ULAYA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini Tanzania (TAFIRI), Daktari Sihaba Mwaitega (Wa kwanza kushoto), amepokea wageni kutoka Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Afisa Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Any Correia Freitas (Wa pili Kushoto) wamefanya ziara kwa lengo la kufanya mazungumzo ya ushirikiano katika utafiti, hususani katika eneo la uchumi wa bluu. Mazungumzo hayo yamejikita katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufugaji wa samaki, mialo, kilimo cha ufukweni, na masuala yanayohusiana na bahari. .

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 28 Mei, 2024, katika ofisi za makao makuu ya TAFIRI, zilizopo Kunduchi, Dar es Salaam.

Post a comment