Dar es Salaam, Julai 2, 2024 – Naibu Makatibu wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (kulia) Dkt. Edwin Mhende (Uvuvi) na (kushoto) Prof. Daniel Elius Mushi(Mifugo), wametembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati wa maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2024) yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Naibu Makatibu Wakuu hao wamejionea bidhaa zitokanazo na mazao ya uvuvi pamoja na teknolojia zitokanazo na tafiti bunifu kama vile teknolojia ya kichanja cha kukaushia dagaa, jiko la kubanikia samaki pamoja na teknolojia ya kuvua na kuuza kidigitali.
Post a comment