TAFIRI YASHIRIKI MKUTANO WA TATHMINI YA MAZINGIRA YA UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA

Dar es Salaam, Julai 16, 2024 – Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Tafiti na Uratibu, Dkt. Mary A. Kishe (wa tano kutoka kushoto), pamoja na baadhi ya watafiti wa TAFIRI walihudhuria mkutano wa wadau kujadili tathmini ya mazingira kimkakati kwa ajili ya programu ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba. Mkutano huu ulifanyika kwenye Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.

Mkutano huu uliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Tathmini ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Deogratius Eugen Paul (wa sita kutoka kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi. Aidha, Mkutano huu ulihudhuriwa na Dkt. John Mapunda (wa nne kutoka kushoto) aliyemwakilisha Mkurugenzi wa ukuzaji Viumbemaji, Dkt. Nazael Madalla (Hayupo kwenye Picha) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Washiriki wote walipata fursa ya kujadili taarifa ya Tathmini ya Mazingira (SEA) kwa ajili ya programu husika na kutoa maoni yao kwa kina.

Post a comment