TAFIRI NA CHUO KIKUU CHA ZURICH WATOA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI ZIWA TANGANYIKA

Kigoma, Tanzania – Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwa kushirikiana na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Zurich cha nchini Uswisi, imeandaa mafunzo maalum juu ya ufugaji wa samaki aina ya ngege wa Ziwa Tanganyika (Oreochromis tanganicae). Mafunzo haya yamehudhuriwa na wafugaji wa samaki kutoka maeneo mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na baadhi kutoka Ziwa Victoria mkoani Mwanza kuanzia tarehe 15 hadi 19 Julai, 2024.

Katika mafunzo haya ya siku tano, washiriki wamejifunza masuala mbalimbali muhimu kwa ajili ya kuboresha ufugaji wa samaki, yakiwemo biolojia ya samaki, mifumo ya ufugaji, ubora wa maji, sheria na miongozo, ukuaji wa samaki, chakula na ulishaji, magonjwa na udhibiti wake, uhusiano wa ufugaji na mazingira, pamoja na uandishi wa andiko la kibiashara (Business plan development).

Mafunzo haya yamefanyika katika viwanja vya TAFIRI Kigoma na yanalenga kuanzisha na kuendeleza ufugaji wa samaki kwa njia endelevu, ili kuchangia katika kuinua uchumi na kuboresha lishe kwa jamii zinazozunguka Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria. .

Post a comment