TAFIRI YASHIRIKI WARSHA YA TAKSONOMIA YA SAMAKI NCHINI AFRIKA KUSINI

Watafiti wa TAFIRI kituo cha Dar es Salaam, Dkt. Mathew Silas, Bw. Godfrey Rusizoka na Bw. Patroba Matiku wameshiriki warsha ya Taksonomia ya samaki iliyofanyika SAIAB (South African Institute for Aquatic Biodiversity) Grahamstown (Makhanda) nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 8 – 19 Julai 2024. Warsha hii pia ilihudhuriwa na washiriki 2 kutoka Kenya, 5 Msumbiji, 1 Urusi na 1 kutoka FAO, Italia.

Lengo la warsha hii ilikuwa ni kujenga uwezo wa kutambua aina ya viumbe maji mbalimbali hasa "faunistic relevance" kama vile aina mpya au rekodi mpya za samaki kwenye eneo la ukanda wa Pwani ya nchi za Tanzania, Msumbuji na Kenya.

Aidha, warsha hii pia ilikuwa na lengo la kuboresha takwimu za samaki ambazo zimekuwa zikitumwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (Food and Agriculture Organization - FAO). Warsha hii itasaidia uboreshaji wa mikakati ya kikanda ya usimamizi hususani kwa samaki waliopo hatari kutoweka na utambuzi wa Bioanuwai zingine kwa ujumla. Warsha hii iliandaliwa na kufadhiliwa na FAO kwa kushirikiana na Taasisi ya Africa Kusini inayohusiana na Bioanuwai za Maji (SAIAB). .

Post a comment