TAFIRI YASHIRIKI MKUTANO WA WADAU WA KUSINI MWA AFRIKA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU MOMBASA, KENYA

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), kupitia mradi wake wa MarCOSIO, inashiriki kikamilifu katika mkutano muhimu wa wadau wa Kusini mwa Afrika unaofanyika Mombasa, Kenya, kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba 2024. Mkutano huu umeandaliwa kwa msaada wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya chini ya mradi mkuu wa GMES Africa, ambao unalenga matumizi ya teknolojia ya Uangalizi wa Dunia (EO) katika maendeleo ya uvuvi na bahari.

Wakati wa mkutano huu, Mhandisi, Innocent Sailale (Kwanza kushoto) na Dkt. Happy Kokwenda (Saba kutoka kushoto) kutoka TAFIRI wamewasilisha mfumo wa PFZ (Potential Fishing Zone), zana muhimu inayowawezesha wavuvi kubaini maeneo bora ya uvuvi kwa ufanisi zaidi, na pia kutangaza kidigitali mavuno yao ili kuongeza fursa za masoko na hivyo kuboresha uchumi wa sekta ya uvuvi.

Taasisi nyingine zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na Baraza la Utafiti wa Sayansi na Viwanda (CSIR) na mpango wa SASSICAL, ambazo pia zinaonyesha mafanikio yao katika matumizi ya teknolojia za kisasa za Uangalizi wa Dunia kwa ajili ya maendeleo ya sekta za uvuvi na bahari katika kanda ya Kusini mwa Afrika.

Post a comment