Mnamo Octoba 25 2024, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) iliwasilisha matokeo ya utafiti kuhusu taarifa ya hali ya uvuvi wa Dagaa wa Ziwa Victoria.
Utafiti huu uliangazia masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii, lishe na kijinsia yanahohusiana na Uvuvi wa Dagaa ambao ni muhimu kwa uchumi wa jamii zinazozunguka ziwa Victoria. Timu ya wataalamu, ikijumuisha Joseph Luomba, Fenant Mhagama na Kalwa Khamis, iliongoza zoezi la uwasilishaji wa matokeo ya Utafiti kwa Wadau wa uvuvi wa Dagaa katika mwalo wa Masonga, Wilayani Rorya. Mkutano huu, ulitoa fursa kwa wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa uvuvi wa dagaa wakiwemo wavuvi, wafanyabiasha na wachakataji wa mazao ya dagaa pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi (BMU) katika kupokea matokeo ya utafiti na kujifunza mbinu bora za kudumisha uvuvi endelevu ili kuhakikisha manufaa ya kiuchumi yanapokelewa kwa usawa na kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa sekta ya uvuvi wa Dagaa inamchango mkubwa katika pato la kaya na imetoa fursa za ajira kwa kundi kubwa la vijana na wanawake ambao wanajihusisha na shughuli za uvuvi ziwani na uchakataji wa mazao ya dagaa. Vilevile sekta imechangia katika upatikanaji wa lishe bora hasa kwa kaya maskini. Hatahivyo, jamii kubwa ya wavuvi bado hainauelewa wa kutosha kuhusu faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa dagaa. Aidha, sekata inakabiliwa na changamtoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa masoko ya kudumu, miundombinu, na kutokuwepo kwa uwiano sawa wa kijinsia katika sekta. Hata hivyo, Bw. Fenant Mhagama (Mbele) akiongoza zoezi la uwasilishaji wa matokeo ya utafiti, alisisitiza kuwa matokeo haya yanatoa mwanga juu ya fursa za kuboresha ustawi wa jamii kupitia uwiano wa usawa wa kijinsia, teknolijia za kisasa za uchataji, taarifa za uhakika za masoko, na mbinu za uvuvi endelevu zinazolenga kuhifadhi mazingira. Kwa upande wao, wadau walionesha kufurahishwa na kitendo cha kupata mrejesho wa taarifa za kitafiti ambazo zimeonesha kuwa na mchango mkubwa katika kujenga uelewa kuhusu uvuvi endelevu na uthabiti wa kiuchumi, lishe na uhamasishaji wa usawa wa kijinsia katika jamii za wavuvi wa ziwa Victoria
Post a comment