MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA WA TAFIRI, GASPER MREMA, AMEONGOZA MAFUNZO YA MAANDALIZI YA MPANGO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2025/2026

Leo, tarehe 23 Januari 2025, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Gasper Mrema (CPA), watatu kutoka kulia mstari wa mbele, amewaongoza wafanyakazi wa TAFIRI kwenye mafunzo yaliyofanyika ofisi ya TAFIRI Dar es Salaam, kupitia muongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/2026. Mafunzo hayo yameendeshwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kupitia Mchumi Mwandamizi, Elias Mafwele, watatu kutoka kushoto mstari wa mbele, na amevaa shati jeupe.

Post a comment