Leo, tarehe 14 Novemba 2023, Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii, Kilimo na Biashara, Baraza la wawakilishi Zanzibar Bi Mtumwa Yusuph (watatu kutoka kulia) akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati hiyo, wamefanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) iliyopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Lengo la ziara hii lilikuwa ni kupata ufahamu wa jinsi TAFIRI inavyofanya shughuli zake za utafiti katika maeneo ya Bahari na maziwa makuu.
Katika ziara hii, Kamati ilipata fursa ya kutembelea maabara ya utafiti katika kituo cha TAFIRI Dar es Salaam. Wajumbe walipata nafasi ya kufahamu mbinu na taratibu zinazotumiwa katika kufanya utafiti, pamoja na kuona matumizi ya vifaa vya kisasa katika maabara hizo. Bi. Fatuma, akizungumza baada ya ziara hiyo, alielezea kuridhishwa kwake na juhudi zinazofanywa na TAFIRI katika kukuza ujuzi na utafiti katika sekta ya uvuvi. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa TAFIRI na ZAFIRI (Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Zanzinbar) katika kusaidia maendeleo ya sekta ya uvuvi kwa manufaa ya jamii na uchumi kwa ujumla.
Ziara hii imekuwa hatua muhimu kuelekea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na taasisi za utafiti, huku ikitoa fursa kwa viongozi kujifunza na kuchangia katika maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini.
Post a comment