TAFIRI KUANZISHA MRADI MPYA WA TATHMINI YA MAVUVI KWA NJIA YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI(eCAS)

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imeanzisha mradi mpya wa tathmini ya mavuvi kwa njia ya kielektroniki kupitia ufadhili wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO). Lengo la mradi huu ni kuendeleza mfumo wa kielektroniki wa tathmini ya mavuvi ya samaki uitwao electronic catch assessment (eCAS) wenye uwezo na mabadiliko ya kuhifadhi data za tathmini ya mavuvi ya samaki. Mkutano wa kuanza mradi huo ulizinduliwa na Mkurugenzi Mkuuu wa TAFIRI, Dkt. Kimirei katika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es salaam. Mradi huo unalenga kukusanya tathmini ya mahitaji ili kuboresha mfumo huo hususani katika ziwa Tanganyika. .

Kulingana na maelezo yaliyotolewa, lengo kuu la mradi huu ni kusaidia sekta ya uvuvi kupunguza gharama za ufuatiliaji wa rasilimali za uvuvi na kutoa maarifa kuhusu viwango vya utumiaji wa rasilimali hizo, ili kuhakikisha matumizi endelevu na yenye faida ya rasilimali za uvuvi. Mfumo huo pia utakuwa na umuhimu mkubwa katika tathmini ya ufanisi wa sera za uvuvi na kufuatilia utendaji wa usimamizi wa uvuvi kwa ufanisi zaidi.

Post a comment