TAFIRI YAWASILISHA MATOKEO YA UTAFITI WA NYAVU ZA ZIWA TANGANYIKA KWA KWA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei akiwasilisha kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (hayupo pichani) taarifa ya matokeo ya utafiti wa nyavu za Freemayaa kwa Ziwa Tanganyika uliofanywa na TAFIRI kwa kushirikiana na Wavuvi wa Ziwa Tanganyika.

Pia mawasilisho hayo yalihudhuriwa na sehemu ya wataalamu wa Sekta ya Uvuvi wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa na TAFIRI kwa kushirikiana na Wavuvi wa Ziwa Tanganyika. Uwasilishaji huo umefanyika katika ofisi za Wizara zilizopo kwenye Jengo la NBC jijini Dodoma Aprili 24, 2024.

Post a comment