UZINDUZI WA KAMPENI DHIDI YA USUGU WA DAWA KWA BINADAMU, MIFUGO NA SAMAKI

Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini Tanzania (TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei (wa pili kushoto) akimwakilisha Katibu Mkuu (KM), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, alihudhuria tukio la uzinduzi wa Kampeni ya Holela Holela Itakukosti, inayolenga kupambana na usugu wa dawa za antibiotics na magonjwa ya zuonotiki. Uzinduzi huo umefanyika siku ya Jumamosi, tarehe 25 Mei 2024 katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam .

Katika hotuba yake, Dkt. Kimirei alitoa mwito kwa sekta mbalimbali kushirikiana katika kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) au Anti-Microbial Resistance (AMR) kwa binadamu, mifugo, na samaki. Kwa niaba ya KM, Dkt. Kimirei aliwaeleza washiriki kuwa, pamoja na mambo mengine, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshaanza kushughulikia masuala haya kwa kutenga fedha za kuzalisha chanjo na kufanya kampeni kubwa ya kitaifa kupambana na magonjwa ya kipaumbele ya mifugo. Magonjwa haya yote yamo kwenye mpango mkakati wa kupambana na UVIDA na magonjwa ya zuonotiki.

Aliongeza kuwa ushirikiano na juhudi za pamoja ni muhimu ili kufanikisha malengo ya kampeni hii na kuhakikisha afya bora kwa binadamu na mifugo nchini Tanzania .

Post a comment