TAFIRI NA KIOST WATIA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA SAYANSI YA BAHARI NA UCHUMI WA BULUU

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei (kushoto), akitia saini Hati ya Makubaliano na Taasisi ya Sayansi ya Bahari na Teknolojia ya Korea (Korea Institute of Ocean Science and Technology - KIOST) kuhusu mashirikiano katika Sayansi ya Bahari na Uchumi wa Buluu.

Hafla ya kutiliana saini ilifanyika katika ofisi za KIOST zilizopo katika Jiji la Busan. Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI alisaini pamoja na Rais wa KIOST, Dkt. Hyi-Seung Lee (kulia) na ilishuhudiwa na DKt. Emmanuel Sweke, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority - DSFA) (Hayupo kwenye picha) na Mr. Paul Makang'a, Mwanasheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Hayupo kwenye picha).

Makubaliano hayo yataongeza tija katika sekta ya uvuvi nchini, pia kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia bahari. Sherehe hiyo imefanyika leo tarehe 3 Mei 2023, jijini Busan. .

Post a comment