NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI (UVUVI) ATEMBELEA TAFIRI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede (wa pili kutoka kushoto), akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh (wa tatu kutoka kulia),pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Neema (wa tatu kutoka kushoto) walitembelea Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI).

Kwa pamoja walipata fursa ya kuzungumza na menejimenti ya TAFIRI pamoja na watumishi wa Makao Makuu na Kituo cha Utafiti cha Dar es Salaam. Vivyo hivyo, walipata fursa ya kutembelea maabara na kuona vifaa vya kisasa vinavyotumika katika utafiti, ugunduzi, na uchakataji wa sampuli mbalimbali, ikiwemo vinasaba vya samaki na viumbe wa majini, ubora wa maji, na madini tembo. Pia walijadili kuhusu kuandaa andiko la mradi kuhusu tafiti zijazo zitakazoweza kutumia maabara hiyo

Post a comment