Leo Tarehe 06 Agosti, 2024: Shule za sekondari kutoka katika jiji la Dodoma zimetembelea Banda la Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) katika maonesho ya NaneNane yanoyoendelea Jiji Dodoma. Shule hizo zimevutiwa na tafiti bunifu zilizofanywa na TAFIRI, ikiwemo teknolojia ya kutambua maeneo yenye samaki wengi 'Potential Fishing Zone' (PFZ).Teknoloji hii itamsaidia mvuvi kuondokana na uvuvi wa kuwinda badala yake itamwezesha kuvua kisasa, kupata samaki wenye tija, na pia kupunguza rasilimali ikiwepo mafuta na muda. Mtafiti kutoka TAFIRI, Mr. Hiari Chona, alipata fursa ya kuwaelezea wanafunzi jinsi teknolojia hiyo ilivyofanikiwa na kuleta tija kwa wavuvi wadogo ukanda wa kusini mwa Bahari ya Hindi. Mr. Chona aliongezea kuwa teknolojia ya mfumo huu inawasaidia pia wachuuzi na wavuvi kuuza au kununua samaki kupitia mfumo huo. Wanafunzi walionyesha shauku kubwa na kueleza kuwa teknolojia kama hizi zinaweza kuboresha maisha ya jamii zao na kuhamasisha uvumbuzi zaidi katika sekta ya uvuvi. Maonesho hayo yalionyesha wazi jinsi sayansi na teknolojia zinavyoweza kubadilisha maisha na kuboresha uchumi wa wavuvi wadogo wadogo.
Post a comment