Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dkt. Ismael A. Kimirei (PhD) (wa tatu kutoka kushoto, mbele), pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha TAFIRI Mwanza, Dkt. Benedicto B. Kashindye (PhD) (wa tatu kutoka kulia, mbele), wamepokea timu ya wataalamu kutoka Jimbo la Jiangsu, China. Timu hii ilitembelea Kituo cha TAFIRI Mwanza kwa madhumuni ya kuandaa ujio wa Gavana wa Jiangsu, ambaye anatarajiwa kutembelea jiji la Mwanza mnamo Oktoba au Novemba 2024. Katika ziara hiyo, Dkt. Kimirei aliwapa wageni maelezo ya kina kuhusu kazi na miradi inayotekelezwa katika Kituo cha Mwanza. Aidha, aliwapeleka kutembelea majengo ya Mradi wa Atamizi Maalumu na Maabara ya Kituo. Kituo cha Mwanza ni miongoni mwa wanufaika wa ushirikiano huu kupitia maboresho yanayotarajiwa ya maabara na mafunzo.Leo Tarehe 16 Agosti, 2024
Post a comment