Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kutoka Makao Makuu na Kituo cha Dar es Salaam, pamoja na watumishi kutoka Idara ya Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wamepokea misheni ya Benki ya Dunia katika ofisi za TAFIRI zilizopo Kunduchi, Dar es Salaam. Ziara hiyo muhimu imefanyika leo tarehe 29 Agosti 2024. Lengo la ziara hii lilikuwa ni kujadili mafanikio ya miradi ya utafiti iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia na kuangalia namna bora ya kutekeleza mradi mpya wa TASFAM ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Katika ziara hiyo, wajumbe wa Benki ya Dunia walipata fursa ya kutembelea na kujionea maabara ya kisasa ya TAFIRI, ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Aidha, walishuhudia mafanikio ya tafiti mbalimbali zinazotekelezwa na TAFIRI, hatua inayodhihirisha ushirikiano wenye tija kati ya taasisi hiyo na Benki ya Dunia. Misheni hiyo ya Benki ya Dunia iliongozwa na TTL wa Benki ya Dunia, Tanzania, ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waliopata fursa ya kuona maendeleo ya utafiti na miundombinu ya kisasa inayotumika katika kuendeleza sekta ya uvuvi nchini Tanzania.
Post a comment